Taarifa
kuwa dereva wa taxi nchini Afrika Kusini alikufa kufuatia tukio la
kufungwa pindu kwenye gari la polisi na kuburutwa mitaani.
Polisi
nchini humo imeanzisha uchunguzi kubainisha ukweli wa tukio hilo ambalo
limetokea katika mji wa Daveyton mashariki mwa jiji la Johannesburg.
Taarifa
za awali kutoka katika vyombo vya habari vya Afrika Kusini zilisema
kuwa polisi walimfanyia ukatili dereva huyo mwenye umri wa miaka 27
kutoka Msumbiji, wakimtuhumu kuegesha gari lake vibaya.
Picha
za video zilizochukuliwa kwa kutumia simu ya mkononi, zilionyesha umati
wa watu ukiangalia, huku maafisa wa polisi wakimfunga mtu huyo kwenye
gari na kuondoka kwa kasi, wakimvuta barabarani.
Inaaminika kuwa mtu huyo alikufa baadaye akiwa kizuizini.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amekilaani kitendo hicho akisema hakikubaliki.
Tazama Video ya tukio hilo hapo chini.