Blogger Widgets
Showing posts with label Makala Maalum. Show all posts
Showing posts with label Makala Maalum. Show all posts

May 18, 2014

Unajua Kama Kumpigia Kura Diamond Platnum ni Simple Sana Hebu Click Hapa ili Umpigia Kura kwenye Tuzo za BET Awards Ikiwa Mpaka sasa Anaongoza

 
Huku akiwa anasuburia kunyakuwa tuzo za MTV zinazotarajiwa kufanyika tarehe 7 june, Diamond amechaguliwa kuwania tuzo za BET katika category ya "Best International Act (Africa)
Diamond anachuwana na mwanadada Tiwa Savage (Nigeria), Davido (Nigeria), Mafikizolo (South Africa), TOOFAN (Togo) na Sarkodie (Ghana)
Diamond anasema hakutarajia kabisa kama angechaguliwa katika tuzo hizo kwasababu hajawahi kuwasiliana nao hata siku moja. Akiongea kutoka London amesema wakati yuko set akiendelea na ku record video yake mpya, manager wake Babu Tale ndio alimwambia

May 6, 2014

Huyu Ndio Mkenya anayeishi kwa Kutegemea Kucha zake na amefanikiwa kufuga kucha zake kwa muda wa miaka 12 na kufikia urefu wa futi moja na inchi 3.



John Waweru akionyesha kucha zake ambazo huzitunza kuliko kitu chochote.

Inaweza kuonekana kuwa ni kitu cha ajabu kwa binadamu wa kawaida kukaa bila kukata kucha kwa mwaka moja, lakini kumbe inawezekana kabisa mtu kufuga kucha kwa muda wa miaka 12.

Hilo limedhihirishwa na John Waweru, raia wa Kenya ambaye amefanikiwa kufuga kucha zake kwa muda wa miaka 12 na kufikia urefu wa futi moja na inchi 3.

Katika mahojiano yake na gazeti la Nairobi News, Waweru anaweka bayana kuwa kucha hizo ndizo zimekuwa chanzo kikuu cha kumwingizia kipato.

Anasema amefanikiwa kuzigeuza kucha hizo kuwa mojawapo ya kivutio cha utalii nchini Kenya kutokana na kuwafanya watalii kuzishangaa na hivyo kumpatia pesa kama malipo ya kivutio hicho.

Ili kuzidi kuwavutia watalii Waweru amezipaka kucha zake rangi zilizopo katika bendera ya Kenya hali inayomwongezea mvuto zaidi.

“Nimezipaka rangi ya bendera yetu kwa kuwa watalii wengi wanaokuja kupiga picha na mimi wanazipenda rangi hizo ili kuwafurahisha wateja wangu,” anasema Waweru akiongea na Kenya News

Anasema siku biashara ikiwa nzuri ana uhakika wa kurudi nyumbani na Sh5,000 (sawa na Sh94,000 za Kitanzania).

Waweru (33) anasema tangu mwaka 2002 alipoanza kufuga kucha hizo hajawahi kuzikata wala kuzipunguza kutokana na sababu yoyote ile.“Baada ya kumaliza shule nilipata kazi lakini kucha zikawa zinakua kwa kasi kiasi cha kunifanya nishindwe kutimiza majukumu yangu nikaona bora niache kazi ili ziendelee kukua bila kikwazo chochote, nazilinda sitaki zikatike kwa namna yoyote.”


May 5, 2014

Tazama Maajabu Mengine Yaliyoibuka Bada ya Diamond Platnum Kuchukua Tuzo saba za Kil Music Awards

Kutokana na Tuzo saba za Kili Music Award zilizofanyika Juzi ambazo Amepata Msanii Daimond Platnum Kutoka  Kundi wa Wasafi Baby. Sasa Maajabu Mapya yameikuka kutokana na Idadi ya Hizo Tuzo, kwani Idadi ya Tuzo Hizo Zimeendana Kabisa Na Idadi ya Maandishi ya vitu vilivyofanya achukue Tuzo Ikiwemo Jina Lake Pamoja na Nyimbo Zake
 Jina lake DIAMOND= Lina Herusi Saba sawa na Tuzo Saba alizopata
Nyimbo Yake NGOLOLO=Ina Herusi Saba sawa na Tuzo Saba alizopata
Au NUMBER 1=Ina Herusi Saba sawa na Tuzo Saba alizopata

TAZAMA PICHA ZIKITHIBITISHA MAAJABU HAYA YA DIAMOND PLATNUM
 1.Jina Lake Lenye Herufi saba sawa na Tuzo Alizopata
  

2.Nyimbo ya Ngololo yenye maandishi saba sawa na Tuzo Alizopata
 b

3.Jina Kamili ya Nyimbo Huyo Number1
 

March 16, 2014

Tazama Picha mbalimbali za story ambayo imesambaa Juu ya kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi kwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Rose Kamili, ambaye pia ni mke wa Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa kwa shutuma ya Rushwa

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza na wanahabari jioni ya leo mara baada ya tukio hilo la kukamatwa kwa Mbunge wa CHADEMA akigawa fedha kwa wanakijiji siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika.Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika kesho siku ya jumapili,ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

 Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga,Iringa Vijijini,Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili amekamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akigawa Fedha kwa wanakijiji hao,akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.


Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akielekezwa sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.


 Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.


Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji 



Gari ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria.


Baada tu ya kukamatwa live akitoa rushwa!! Mbunge Rose Kamili wa Chadema!
credit: michuzijr blog

March 6, 2014

Tazama Huyu Msanii wa Kike wa Bongomovie alivyopiga Picha za Kuwatega Wanaume na kuziruhusu kwenye mitandao..KISA?

Star wa filamu anayekimbiza sokoni kwasasa na filamu kibao Mariam Ismail ameonekana kuweka mapozi ya Ajabu katika picha zake mpya kama anavyoonekana hapo chini........


February 28, 2014

Tazama Pica za Wasani wa waliozindua kampeni ya kitaifa kuishinikiza serikali kuwatambua katika katiba


Leo asubuhi  (February 28) pande za Kinondoni Vijana Social Hall kulikua wasanii wa fani mbalimbali waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kuzindua kampeni ya kitaifa maalum kwa ajili ya kuishinikiza serikali kuwatambua wasanii kikatiba.
Licha ya kuwa na shinikizo hilo lakini pia kutakuwa na  maandamano ya amani wanayotarajia kuyafanya ikiwa ni sambamba na kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kumteua mmoja wao (hajafahamika bado) washiriki kuhudhuria katika bunge la katiba.
tumepiga na nikki wa pili moja kati wasanii waliopo mstari wa mbele kwenye movement hii



"Tumezindua kampeni yetu ya kitaifa kushinikiza serikali itambue wasanii kama kundi maalum kwenye jamii na kuingizwa kwa haki bunifu katika katiba hizo ndio hoja zetu mbili tunazozipigia kelele" amesema Nikki wa Pili 

Tazama Picha za Wasani wa waliozindua kampeni ya kitaifa kuishinikiza serikali kuwatambua katika katiba.Huku Proffesa Jay,Huku Pfunk,Nick wa Pili na wengine Kibao

Je kuna kitu unaweza kukisema kwenye barua ya kuomba kazi na kikakuhakikishia wewe kutimiza malengo yako na kukupelekea kuitwa kwenye usaili?
yolanda-spivey_black-woman-pretends-to-be-white-to-get-job1
Barua ya kuomba kazi inaongelea kwa kifupi kuhusu wasifu wako na kukujumuisha kama mtu anayehitajika kwenye kazi furani.
Ni sehemu pekee ya kuonyesha unahitaji hiyo nafasi ya kazi na kutengeneza uhusiano wako na mwajiri mtarajiwa. kuonyesha kwamba unahitaji kazi hiyo kwenye barua ni muhimu sana, na kuna jambo moja linalokuhakikishia utaitwa kwenye usaili.

Omba kukutana na Mwajili au Mtu anayefanya Usaili.

Je waujua usemi unaosema, ‘Ombeni nanyi mtapewa’? Ni kweli. Linaweza kuwa jambo la kawaida na ushauri wa kawaida bali ni mara ngapi umeandika barua ya kuomba kazi bila kuomba kufanyiwa usaili? wakati ni rahisi kufanya!
Wakati unamalizia kuandika barua yako, kitu unachotakiwa kukifanya ni kumuuliza mwajiri kuhusu kukwita kwenye usaili. Utafiti unaonyesha watu wanaoandika kwenye barua na kuomba kufanyiwa usaili wana nafasi zaidi ya kuitwa kuliko ukinyamaza kimya.

February 3, 2014

Picha Jinsi CCM Ilivyochukua karibu nusu ya wasanii wa Bongo Movies, wapo JB, Uwoya na wengine


Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM jioni ya leo

Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.


Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia Wananchi na Wanachama wakereketwa wa chama hicho,mapema leo jioni kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea kilele cha miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo.

Sehemu ya Umati wa Watu waliofika kwenye shamrashamra hizo leo.

Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika jembe na nyundo,ikiwa ni alama ya Mkulima na Mfanyakazi mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hil
Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.
 
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi ya gitaa Msanii maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awil,anaeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi.Zakia Meghji.

January 11, 2014

Haina Ubishi: Huyu Ndio The Real Boss Lady Kwa Africa Mashariki


 







Zari ni mrembo mwenye makazi yake Africa Mashariki katika nchi ya Uganda, Ni mrembo haswa mwenye umate mate wakutosha wa kumwezesha kumiliki Usingizi mzuri magari ya kifahari yani full kipupwe. Maisha ya raha kwake ni sawa na doze anaweza kufanya chochote kwani umate mate unaongea. Lakini je umate mate huu umetokana na nini mimi na labda na wewe tutabaki kujiuliza bila majibu lakini mwenyewe anajua . 
Zari akiwa kajipumzisha nyumbani kwake, Jitiririshe chini
Huu ndiyo usingizi wake full kipupwe 
Unaweza kuona na kutambua kuwa kizuri kula na ndugu zako 
Usafiri wa kwendea sokoni ni habari ya mjini
Usafiri wa kwendae duka
Huu ni usafiri wa kwendea kwenye shughuri za kioffice 
Zari akiwa ndani ya duka lake la vito vya thamani
Habari ndiyo hii najua ungetamani kuweka kioo chuni kwa wale wa tuliosoma shule zetu za uswahili kama mimi jibu mnalo..tee tee tee tee...!!

December 10, 2013

Matrida ndio Msichana Anayefuata Nyayo Za Rihanna Kwa Kuachana Picha za Ajabu and She Dont Care


Wakati mwingine unaweza ukakutana na Mwanamke wa aina ya pekee na uzuri wake ukakufanya mwanaume ukose la kuongea, sijui kwa wanaume waliokamaliki hili mnalionaje, naomba niwatambulishe kwenu Maltilda Quaye a.k.a Hipsy, ni mwanachuo kutoka nchini Ghana ambaye anachipukia kwa kasi ya umeme katika masuala ya Urembo na kuonekana katika Videos mbalimbali. Kweli hizi ni Hips dont lie, angalia picha 7 zaidi hapo chini.