Blogger Widgets
Showing posts with label Siasa. Show all posts
Showing posts with label Siasa. Show all posts

March 16, 2014

Tazama Picha:Diwani wa ccm akamatwa ana kadi feki za chadema zikiwa na saini ya Mh Mbowe

 
Kadi feki za CHADEMA alizokutwa nazo
Diwani wa viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kalangalala na tarafa ya Geita wilayani Geita mkoani Geita Zaitun Sued Fundikira  anayeishi katika mtaa wa Mission.
Kadi feki za CHADEMA zikiwa na saini ya mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe.
======
 
Diwani wa viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kalangalala na tarafa ya Geita wilayani Geita mkoani Geita Zaitun Sued Fundikira  anayeishi katika mtaa wa Mission amekamatwa na kadi za kugushi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kadi zilizogushiwa ni 23 zikiwa na saini ya mwenyekiti CHADEMA taifa Freeman Mbowe,kadi ambazo hazijaandikwa chochote katika baadhi ya sehemu kama vile jina la mwanachama na sehemu anayokaa.

Wakisimulia juu ya tukio hilo mashuhuda walisema kuwa mnamo saa nne asubuhi alitokea mtoto mmoja akiwa na kadi za Chadema amezishika mkononi akitembea nazo mtaani na kutokeza katika kijiwe cha Kalakana ya wakereketwa wa Chadema maarufu kama “Kijiwe cha Sengerema” ndipo walipomuona mtoto huyo walipomuuliza akasema kuwa amezitoa ndani kwani zimo nyingi sana.

Mara baada ya kuambiwa hivyo wakamwambia mtoto huyo awapeleke na mtoto huyo aliongozana nao hadi nyumbani kwa diwani huyo na walipofika ,mtoto aliingia ndani na kuwaletea kadi nyingi mkononi huku akiwa na mkoba umejaa kadi zingine.

Muda mchache tu baada ya mtoto kutoka na kadi hizo huku wakereketwa hao wakizichukua ghafla diwani huyo alijitokeza nje huku akihaha na kufoka kuwa hizo kadi hazijui.

 “Nashangaa mimi kadi hizi sizijui kabisa licha ya kuwa kwenye mkoba wangu lakini sijui nani aliyeziweka humu,na mwandishi yeyote atakayeniandika nitamshtaki’’,alieeleza diwani huyo.

Taarifa za kuaminika kutoka kwa wananchi wamesema kuwa diwani huyu amekuwa akiratibu shughuli mbalimbali za kutaka kudhoofisha Chadema katika eneo hilo ambapo inadaiwa kuwa hadi kombati za Chadema zimeshaandaliwa ikiwa ni pamoja na kadi hizo feki kwa ajli ya kuhakikisha ujio wa aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe atakapokuja kanda ziwa wapewe watu kadi hizo na kuvulishwa kombati za chama ili watamke kuwa wamejitoa Chadema.

Tazama Picha mbalimbali za story ambayo imesambaa Juu ya kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi kwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Rose Kamili, ambaye pia ni mke wa Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa kwa shutuma ya Rushwa

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza na wanahabari jioni ya leo mara baada ya tukio hilo la kukamatwa kwa Mbunge wa CHADEMA akigawa fedha kwa wanakijiji siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika.Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika kesho siku ya jumapili,ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

 Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga,Iringa Vijijini,Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili amekamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akigawa Fedha kwa wanakijiji hao,akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.


Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akielekezwa sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini Iringa jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya jumapili.


 Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.


Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji 



Gari ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya kuchukuliwa kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa na uongozi wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria.


Baada tu ya kukamatwa live akitoa rushwa!! Mbunge Rose Kamili wa Chadema!
credit: michuzijr blog

February 3, 2014

Picha Jinsi CCM Ilivyochukua karibu nusu ya wasanii wa Bongo Movies, wapo JB, Uwoya na wengine


Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasanii mahiri wa Filamu hapa nchini,mara baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama cha CCM jioni ya leo

Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.


Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia Wananchi na Wanachama wakereketwa wa chama hicho,mapema leo jioni kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea kilele cha miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hilo.

Sehemu ya Umati wa Watu waliofika kwenye shamrashamra hizo leo.

Mwenyekiti wa chama chama cha CCM,Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshika jembe na nyundo,ikiwa ni alama ya Mkulima na Mfanyakazi mara baada ya kuwasili jioni ya leo kwenye kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho,yaliyofanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine,jijini Mbeya,Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuhudia tukio hil
Katibu wa NEC, Itikadi,na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye akiwatambulisha baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini,ambao kwa nia thabiti wameamua kujiunga na chama hicho,wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB,Blandina Chagula,Mboto,Irene Uwoya,Single Mtambalike na wengineo.
 
Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi ya gitaa Msanii maarufu wa jijini Mbeya,Petrol Abel a.k.a Awil,anaeshuhudia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi.Zakia Meghji.

January 30, 2014

TazamaPicha Jinsi Msani Afande Sele Alivyotambulishwa Rasmi Kama Mwanchama wa CHADEMA na kiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe

 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akimtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Dama, uliofanyika katika Kata ya Tungi mjini Mororgoro .
 Mwenyekiti wa Chama ch Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mtibwa katika mkutano wa Operesheni M4C pamoja Daima.



Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele akiwahutubia wananchi wa Kata ya Tungi mjini Morogoro, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoj Daima.
 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mtibwa, katika mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima.

January 23, 2014

Taswira za Uzinduzi wa Operesheni Pamoja Daima Mkoani Ruvuma,Songea

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa akiwasili Songea.

Dr Slaa akiwahutubia wakazi wa Songea.

Dr Slaa akiwahutubia wakazi wa Mbinga


Dr Slaa akiwahutubia wakazi wa Namtumbo.
Mbunge wa Iringa Mjini Mh Peter Msigwa akiwahutubia wakazi wa Mbinga. 

Msigwa akiwahutubia wakazi wa Songea.

January 9, 2014

Maneno Ya Joyce Kilia Kuhusu Shutuma Ya Zitto Kabwe na Mtazamo wake Juu ya Chuki ya Mh Mbowe

NGUVU YA ZITTO IMEMUINGIA HADI MKE WA JUNIO KILEO,KILEO NI YULE AMBAE ALILALAMIKIWA NA KUSHITAKIWA NA ZITTO KUWA ALIWEKA KWENYE MTANDAO WAKE HABARI ZA KUWA ZITTO KAONGWA NA CCM

MKE WA KILEO BI JOYCE KIRIA AAMUA KUANIKA UKWELI HADHARANI

Dada Joyce Kiria ambaye ni mwendesha kipindi cha Wanawake Live CHA EATV
Haya ndiyo maoni yake katika mjadala mmojawapo katika wall ya Albert Msando. Mjadala upo chini ya Kitila na Mwigamba wavuliwa uongozi.
"Kama CDM mmeamua kuchonga barabara, msiwaache wanaokwenda kinyume na Miiko na Maadili ya Uongozi. Mh Mbowe kazaa nje ya Ndoa! Mh Mukya kazaa na Mume wa mtu. HAO NI VIONGOZI WA AINA GANI??

Na Viongozi wengine wenye tabia za namna hiyo hawafai hata kuwa wajume wa nyumba 10...


CDM Mkiishia kwa ZZK mtakuwa Mmebagua sana. Na mtakuwa mmewaonea sana kina ZZK na his Team. Mtazamo tu


Yangu Macho...


Uaminifu ndo Msingi wa mambo yote! Ukishindwa kuwa mwaminifu kwenye familia yako, Ndoa yako, nyumbani kwako, hakuna mahali pengine utaweza kuwa Mwaminifu.


Hayo ya Ufisadi yanaanza na Mtu binafsi, Familia, ( Mke) na mwisho ndo Jamii...


Umeshindwa kuongoza Familia yako, ivi kweli Taifa ndo Utaliweza??


CDM msipokubali chujio liwapitie wote, mkabakia kuangalia tabaka na vidagaa mtachelewa sana kufika....

January 4, 2014

Tazama Vioja Vilivyotokea Jana Kwenye Kesi ya Zitto Kabwe

 
Dar es Salaam,Tanzania

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe (Chadema), kuhusu ombi la kuitaka Mahakama hiyo kuizuia Kamati Kuu ya Chama hicho, kutomjadili katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika leo jijini Dar es Salaam.




Wanachama wa Chadema, wakitwangana nje ya Mahakama Kuu, jijini Dar es Salaam. 

Jaji John Utumwa alisitisha kutoa hukumu hiyo mpaka siku ya Jumatatu saa 4:00 asubuhi.Hata hiyo baada ya Jaji huyo kuahirisha kesi hiyo, nje ya Mahakama hiyo kulikuwa na vurugu kubwa baada ya kundi linalo unga mkono maamuzi ya Chadema kutwangana na kundi linalo muunga Zitto Kabwe.

 

January 2, 2014

Mchungaji Peter Msigwa asisitiza kuwa Zitto Kabwe ni lazima avuliwe uanachama wa CHADEMA kesho

MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ametaka wana Chadema kuunga mkono mpango wa kumfuta uanachama aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wao, Kabwe Zitto.
“Kuna mlolongo wa mambo yaliyofanya Chadema ikachukua hatua kali dhidi ya Zitto, mambo hayo yamesemwa sana na viongozi wetu; Januari 3, vikao vya chama vitaanza mchakato wa kuhitimisha suala hilo,” alisema.

 “Amekwishaandikiwa barua ya kujieleza kwa nini asifukuzwe uanachama, sasa nawaulizeni wana Chadema Iringa afukuzwe au asifukuzwe ili nikifika kwenye kikao nitoe msimamo wa Iringa?” Aliuliza na sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wake wakijibu “afukuzweeee….”
 
Katika mkutano wake Desemba 31, kwenye Uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa, Mchungaji Msigwa alisema Zitto amekikosea mengi chama hicho, hali iliyowanyima uvumilivu na kuamua kumwondoa katika nafasi zake zote za uongozi.

December 26, 2013

Soma Hi Taarifa ya Msanii wa HIP HOP Roma Kujiunga na Chadema Baada ya Sugu, Soggy, Profesa na Afande sele

Amesema mengi kupitia nyimbo zake na amewahi kukanusha kujiunga na siasa lakini sasa baada ya kuona ujumbe ambao amekuwa akiutuma kupitia muziki umepuuzwa sasa ame..


ROMA MKATOLIKI WA JIJINI TANGA: Akiongea na Mabest zake Wa Mtaani huko Tanga amesema ana mpango Kuingia Kwenye Uringo wa Kisiasa ili apate nafasi Nzuri ya Kuikosoa Serikali baada ya Muziki wake Kupuuzwa na Viongozi wa Taifa hili. "Naplan Kuzamia Kwenye Mambo ya Politics hivi sasa, By the Way Wiki Ijayo naweza Kuchukua Kadi ya Chadema Rasmi"... Pia amesema Atahakikisha Wasanii Wenzake wanaoimba Muziki wa HipHop akina Kala Jeremiah nao Wanaunda timu ya Maangamizi Kuing'oa CCM

December 24, 2013

Soma Jinsi Mama Mjane Samantha Lewthwaite Aliyefanya Shambulia la Kigaidi WestGate Jijini Nairobi Alivyonaswa kwenye Msitu wa nyoka na nge Hatari Akiwa anasafiri na Ngamia

Samantha Lewthwaite.
Mjane mweupe wa Uingereza anaaminika kuwa anasuka mipango mipya ya mashambulio ya ugaidi kutoka kwenye kambi ya mafunzo inayohusishwa na Al Qaeda baada ya kuonekana akiondoka kwa kutumia ngamia katika msitu wa nyoka wa kufugwa nchini Somalia.

Samantha Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 29, anashukiwa kusaidia kuratibu shambulio katika jengo la biashara la Nairobi mnamo Septemba ambalo lilisababisha vifo vya watu 67.
Inaaminika mtuhumiwa huyo wa ugaidi alisafirishwa katika gari la 4x4 kuvuka mpaka wa Kenya kwenda nchini Somalia ambako tangu wakati huo alionekana mara nne.


Kuonekana kwake kwa hivi karibuni kabisa kulikuwa wiki mbili zilizopita, pale mashushushu walipomwona mama huyo wa watoto wanne akiendesha ngamia kati ya kambi za mafunzo mjini Baidoa.
Samantha, mjane wa mmoja wa walipuaji wa 7/7 mjini London, sasa anaaminika kuwa katika kambi ya mafunzo iliyojificha katika msitu huo ambayo inaendeshwa na makundi ya kigaidi yanayohusishwa na Al Qaeda.
Kanali Yasin Hiro wa Jeshi la Serikali ya Somalia alieleza: "Amekuwa akisafiri kwa kutumia ngamia. Tunadhani yuko kwenye kambi hizo. Tunatumaini nyoka hao na nge wanampenda."

November 20, 2013

Tazama Picha Jinsi Afande Sele Alivyopokelewa Na watu Kwenye Hatua Za Kujiunga Na Chadema Huko Morogoro




Mwanamziki mashuhuri Tanzania, anayejulikana kama Afande Sele Amejiunga na M4C, kwa kuingia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Mji wa morogoro ulirindima vifijo wakati Afande akizunguka na Msafara wa Piki Piki kuwaaga rasmi wale wasio na misimamo thabiti Kisiasa, kama inavyoonekana katika picha. kwa upande mwingine wapenzi wa CCM walionekana kuwa nahofu na uchungu, na walihisi sasa mambo yanazidi kuwa magumu sana kwao.

November 14, 2013

Mtazame Mbunge Aliyetuhumiwa Kumbaka Mwanafunzi wa Miaka 16 na Kumuambikiza VVU na Kumtishia Kumuua Endapo Atatoa Siri

Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM). MBUNGE wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), ameingia katika matata. Katika kujaribu kudhibiti mtoto wa shule ambaye anadai alibakwa naye na kuambukiwa virusi vya ukimwi, mbunge huyo ametoa vitisho vya kuua mtoto huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili.

Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti habari za mbunge mmoja (bila kumtaja jina), jana asubuhi Profesa Kapuya ameibuka na kumtisha mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 anayesoma Shule ya Sekondari Turiani iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam.

Baada ya kujua kuwa mtoto huyo ndiye alitoa habari za masahibu hayo, ambayo mbunge hakutaka yajulikane, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.

Jana Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Profesa Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.

Alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993930, Profesa Kapuya alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo: “chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?”

Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: “Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.

“Mwambieni Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si mmemuingizia hela leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote.

“Jana si wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa imeisha, maana wameshatengeneza hela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani anawakamata? Nani atapigana nasi?”

Hata hivyo, baada ya kuhisi kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia hatua, na wamewasiliana na taasisi mbalimbali za kiraia na serikali zenye uwezo wa kumtia adabu, mbunge huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa kuonyesha alikuwa anafikiria kunywa sumu..

November 3, 2013

Soma Alichokisema Kiongozi wa Waasi wa M23 wenye Ukarasa Wake wa Facebook Baada ya Kupotea Kwa Muda Mfupi

Kwa muda mufupi sikupatikana kwenye mutandao wa facebook na kwenye simu, sababu nilikuwa mahali hakuna network, kwa sasa nimefika mahali kuna network, Mutaanza pata habari kwa wakati. hatukupigana, tulijitosha katika maeneo zetu bila kupigana, silaha zetu zote tulienda nazo hakuna yenye tuliaca. Ingelukuwa tulikimbiya hatugepata wakati ya kubeba bitu yetu. sasa mutu mwenye anayuwa fanya analyse, aifanye sasa. 1 kwa nini tilijitosha mumaeneo yetu bila kupigana? 2 Tulienda wapi? 3 Tutabakiya kwenye tulienda ama tutarundi, 3 Mbone FARDC haitufwate kwenye tuko? 4 kwa nini Kabila ameitika kuya zungumuza na japo kuwa

October 29, 2013

Mtazame Sasa Msanii wa Bongo Movie "CHOPA" Akiwa Kwenye Mavazi ya CCM na Kutangaza Nia ya Kugombea Ubunge

Yule msanii wa vichekesho nchini alialeta msemo wa alimashauri ya kichwa bwana juma chikoka alimaarufu kwa jina la chopa mzee wa halimashauri ya kichwa bado ameonyesha kutokukata tamaa katika harakati zake za kuelekea mjengoni mara atakapotwaa kiti cha ubunge.

Chopa ambaye mwaka 2010 aligombea kiti hicho kwa tiketi ya ccm wilaya ya ilala lakini kura hazi kutosha hivyo akawa kashindwa kuendeleza harakati zake za kuingia mjengoni hivyo kwa sasa chopa ameibuka tena na kusema kuwa bado nia nguvu na hari ya kugombea ubunge anavyo na ana uhakika safari hii ni ushindi wa kishindo.

                           
Ujumbe waa chopa katika instagram unasomeka hi ......2010 nligombea ubunge lakin kura hazikutosha,sijakata tamaa na sitakata tamaa ktk mbio za kufikia ndoto zangu, japo kuna watu wazito wameanza mbinu chafu dhidi yangu,wakiendelea ntawataja hadharani..MUNGU nijaalie afya,uwezo, na ujasiri na nguvu koz naamin akuna kinachoshindika kikubwa ni uzalendo,uwezo,mipango na mbinu..aliandika chopa kupitia mtandao wa instagram


October 22, 2013

Picha Zikionesha Jinsi Mh. Jakaya Alivyozuiliwa na Wananchi Kwa Mabango Ili Asikilizwe Kwa Vilio Vyao

Msafara wa JK ukiwa umezuiwa eneo la Mbwila Ludewa leo
 Wananchi  wa Mlangali  wakiwa  wamezuia  msafara wa Rais Kikwete

 Madai  ya  wana Ludewa kwa JK

Msafara  wa JK  ukiwa  umezuiwa  eneo la Mbwila Ludewa leo