Blogger Widgets
Showing posts with label Hip Hop City. Show all posts
Showing posts with label Hip Hop City. Show all posts

May 24, 2014

Hebu Tazama Amazing Pichures za Pre-wedding dinner ya Kanye West na Kim Kardashian iliyofanyika jana Paris, ndoa kufungwa leo (May 24) Italy

Jana Ijumaa (May 23) Kanye West na Kim Kardashian waliianza ratiba yao kuelekea siku ya harusi ya mwaka inayosubiriwa kwa hamu kubwa kwa kufanya ‘pre-wedding dinner party’ huko Paris, Ufaransa huku ndoa yenyewe ikitarajiwa kufungwa leo.
kimye1
Maharusi wakiongea mbele ya wageni waalikwa

Jana mitaa ya Paris ilishuhudia pilikapilika za wageni na mapaparazi wakielekea eneo ilipofanyika sherehe ya chakula cha jioni kabla ya ndoa (pre-wedding dinner), iliyohudhuriwa na wageni wanaokadiriwa kufikia 100 wakiwemo dada zake Kim, Kourtney, Khloe, Kylie, Kendall na mama yake Kris Jenner na wageni wengine mbalimbali.
kimye3
Kim na ndugu zake

Usiku huo ulipambwa na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwimbaji aitwaye Lana Del Rey.
kimye2
Kwa mujibu wa ripoti, fataki zilitawala eneo la tukio, huku ikisemekana anga la eneo hilo siku ya jana lilikuwa ‘NO-FLY ZONE’, hakuna ndege yoyote iliyokatiza.
.
Chupa 1,000 za champagne ziliandaliwa kwaajili ya wageni waalikwa waliohudhuria.

Kwa mujibu wa Entertainment Tonight, maharusi watarajiwa Kimye waliwatangazia wageni waalikwa kuwa ndoa yao itafungwa siku inayofuata yaani leo Jumamosi (May 24) huko Italy.
kimye5
kimye6-kanye akilinda mali yake
Kanye akilinda mali yake

kimye7

March 10, 2014

Pata Muda sasa wa kusikiliza ile ngoma mpya ya Roma K.K.K..Sikiliza alivyoizungumzia "FURSA",Team Anaconda na Jinsi Kundi la watu wanavyoligawa hili soko la mziki


KKK 
Huu ni wimbo wa Roma ambao Teaser yake ilianza kuonekana wiki iliyopita kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii,jina la wimbo unaitwa KKK umefanyika Tongwe Records,kashirikishwa msanii mchanga kabisa kwenye muziki anaitwa Nicolazo ambaye kiasili anatokea Mtwara.
Bonyeza play kusikiliza.

March 8, 2014

Haya Huyu Hapa Roma na Ngoma Yake Mpya ya KKK na Asimulia kuhusu yeye kuingia kwenye siasa

Msanii wa Hip Hop, Roma Mkatoliki amesema kuwa hajawahi kufikiria kama atakuja kuwa mwanasiasa katika maisha yake, ingawa kuna baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wamekuwa wakimtaka agombee Ubunge.
ROMA TUZO
Roma amesema kuwa ameshapokea maoni kutoka kwa viongozi mbalimbali wakimshawishi agombee nafasi ya kisiasa, ila anadai alikataa kwakuwa anatambua nafasi yake ni ipi katika jamii.
“Toka miaka mitano iliyopita nimekuwa nikiendelea kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wasanii wenzangu,wananchi wa kawaida na viongozi wa dini ,viongozi wa serikali, mawaziri wabunge, na kunifuata na kuniambia nigombee ubunge,” ameiambia Bongo5.
“Sijawai kufikiria kuingia katika siasa kugombea ubunge ama kujiHusisha na siasa,napenda nisimame kama msanii kwasababu naamini jukwaa ambalo ninalo ni bora kuliko jukwaa ambalo wanasimama wanasiasa au kuliko mheshimiwa fulani. Mahubiri yangu ninavyohutubia katika muziki inawezekana yana nguvu kubwa kuliko hata mtu fulani, kiongozi ama mbunge wa jimbo fulani. Kwahiyo nafasi ambayo nipo naiona ni nzuri na sijawahi kufikiria kuingia katika siasa.”
ROMA CDM

December 30, 2013

Soma Hapa Habarri Mpya Kutoka kwa Joh Makini na Nikki wa Pili

Rappers ndugu wa kampuni ya Weusi Joh Makini na Nikki wa Pili, mwezi January 2014 wanatarajia kufanya video tatu za nyimbo zao zilizotoka na hazina video mpaka sasa.
Joe Makini & Nikki wa Pili
Joh ameiambia Bongo5 kuwa video ya kwanza wanatarajia kuifanyia jijini Arusha wiki hii na director Nisher, na kuwa wanatarajia kuondoka kesho (Dec 31) pamoja na G-Nako kuelekea Arusha kwaajili ya kazi hiyo.
Amesema video ya pili ambayo itakuwa ya single yake na Nikki wa Pili ‘Bei ya Mkaa’ itafanyika Dar es salaam chini ya muongozaji Adam Juma, katika wiki ya pili au ya tatu ya January.
Makini ameongeza kuwa video ya tatu anayotegemea kuifanya mwezi January mwakani ni ya single yake ‘Nikumbatie’ ambayo audio ilitengenezwa na Fundi Samweli. Joh amesema video ya wimbo huo anategemea kuifanya na director wa nje.

December 18, 2013

Duh! Kanye West afanya Maajabu kwa kundi la watu wanaomfanyia make-up Kim Kardashian

Linapokuja suala la kuhakikisha mama wa mwanae, North anapendeza kadri iwezekanavyo, Yeezy hana mkono wa birika. Na ndio maana ametema $250,000 (zaidi ya shilingi milioni 400) kwaajili ya kundi la watu wanaompamba Kim Kardashian ( glam squad).
article-0-1A29E6FC00000578-403_634x971
Staa huyo amekuwa akisindikizwa na mchumba wake kwenye ziara yake Yeezus nchini Marekani na amehakikisha mtu wa kumpamba nywele Kim (hair dresser) msanii wa make-up na mtu wa mitindo kuitwa muda wowote na mahali popote wanapohitajika kumpamba mrembo huyo kwakuwa amekataa kutumia watu wengine.

Chanzo kimeuambia mtandao wa RadarOnline.com: ‘Kanye amemuambia Kim atatumia kiasi chochote kuufanya muonekano wake tayari kwa upigaji picha mkubwa muda wowote akitaka Hivyo hair stylist wa Kim, make-up artist na mtu wa mitindo wote wanaoishi Los Angeles, wako tayari saa 24/7, kuchukua private jet kumfuata alipo.

December 10, 2013

Tazama Tattoo ya Msanii The Game wa Marekani Yenye Sura ya The Late Nelson Mandela

Hakuna mtu yoyote ambaye hajaguswa na kifo cha Mzee Nelson Mandela kutokana na historia ya pekee aliyoiacha kiongozi huyu wa Afrika Kusini. Kuanzia mataifa ya Asia,Ulaya,Marekani, wanamichezo,waigizaji hadi watu wa kawaida wameonyesha masikitiko yao kwa kumpoteza mfano mzuri kwenye uongozi. Headline mpya inamhusisha msanii nguli wa hiphop The Game ambaye ni mpenzi mkubwa wa tatoo. Hivi sasa amechora tatoo kubwa za sura za wanae,Barack Obama, Trayvon Martin na Nelson Mandela akiangalia nje ya gereza. The game ali-share picha akionyesha tatoo hiyo kubwa na kuandika ,“The finished ‘Nelson Mandela’ lookin out of the prison bars by @NikkoHurtado done on my side. 7 hour sitting…. Few more hours to tie in the tats around it & we solid,”

November 4, 2013

Tazama Alichokifanya Roma Kwenye Makamuzi ya Tamasha la Born Fire Chuo cha Sauti Jijini Mwanza Akisapotiwa Jambo Squard


Roma Mkatoliki alikinukisha kwenye Tamasha la born fire chini  ya Udhamini mnono wa Serengeti Breweries kupitia kinywaji chake cha Pilsner Lager King of Bold, tamasha likifanyika viwanja vya Raila Odinga chuo cha Sauti Nyegezi jijini Mwanza.

Burudani inapokolea....

Hisia za Roma.

aaaaah saa mingi umepanda...!!!

November 3, 2013

Tazama Picha Mbalimbali Jinsi Songa,Fid Q,Damian,Chidi Benz na mwana Dada Rukki walivyopendezesha Show ya WAKAZI

Rapper Wakazi Jumamosi hii alifanya uzinduzi wa video yake mpya, Touch pande za Nyumbani Lounge na kusindikizwa na rappers/wanamuziki wengine wakiwemo Songa,Fid Q,Damian,Chidi Benz na mwana Dada Rukki. Pia kwenye uzinduzi huo trailer ya filamu ijayo iitwayo Going Bongo ilioneshwa. Tazama picha za mambo yalivyokuwa.
IMG_0690
Mwanadaada Rukki akitoa burudani

IMG_0697
IMG_0698
Dancer huyu alitia fora jana

IMG_0699
Fid Q na AY waliamua kwenda kutunza kidogo

IMG_0700
Watu waliouhudhuria wakifuatilia kwa makini

IMG_0712
Damian Soul akiimba kwa hisia

IMG_0719
Songa akitumbuiza

IMG_0724
IMG_0725
IMG_0726

November 2, 2013

Tazama Maangamizi ya Faridi Kubanda.Duhh Huyu Mshkaji Kama Mbele Vile

Kampuni ya Cheusi Dawa ya Fid Q, jana ilifanikisha kwa mara ya tatu kuandaa showya Poetry Addiction aka ‘Uraibu wa Ushairi’ iliyofanyika kwenye ukumbi wa Triniti jijini Dar es Salaam. Show ya jana ilishuhudia wasichana pekee wakitumbuiza wakiwemo, Aichi, Kethi, Charlotte O’Neal maarufu kama Mama C, Jade, Vanessa Mdee, Grace Matata, Elizabeth Mwakijambile na wengine
wajaribu kuwatengenezea mazingira basi’ – Fid Q
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11