Blogger Widgets
Showing posts with label Matukio. Show all posts
Showing posts with label Matukio. Show all posts

June 5, 2014

Picha: Msiba wa Tyson wamaliza ugomvi wa Wema na Kajala? TAZAMA PICHA

Huenda ule ugomvi kati ya Wema Sepetu na Kajala ukawa umeisha kutokana na matukio mbalimbali ya picha hasa za msiba wa George Tyson.
Kajala na Masanja
Kajala na Aunt Ezekiel
Mtandao wa Global Publishers umedai kuwa ugomvi Wema Sepetu na Kajala Masanja umekwisha kufuatia kukalishwa katika kikao cha siri kilichofanyika kwenye msiba wa aliyekuwa muongozaji wa filamu marehemu George Otieno ‘Tyson’.
Aunt Ezekiel,Kajala pamoja na wenzake
Aunt Ezekiel,Kajala pamoja na wenzake
Hata hivyo, katika mazishi ya marehemu Rachel Haule katika makaburi ya Kinondoni Wema Sepetu na Kajala Masanja kila mmoja alikaa kwa kundi lake.
Wema akiwa amekaa na wenzake
Wema akiwa amekaa na wenzake kwenye msiba wa Rachel Haule

June 2, 2014

PHOTO’S: Kili Music Tour yavunja rekodi MWANZA.Tazama Picha Mbali Mbali

BEN POL (1)
Msanii wa Bongo flava, Ben Pol akitumbuiza maelfu ya wakazi wa Mwanza wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Bongo flava artiste Ben Pol entertains thousands of Mwanza residents during the ongoing Kili Music Tour concert held at Kirumba Stadium in Mwanza that attracted thousands of fans. The tour is sponsored by Kilimanjaro Premium Lager.
CHRISTIAN BELLA (2)
Msani wa muziki wa dance, Christian Bella akikonga nyoyo za wakazi wa Mwanza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Renowned artiste Christian Bella doing what he does best during the ongoing Kili Music Tour concert held at Kirumba Stadium in Mwanza that attracted thousands of fans. The tour is sponsored by Kilimanjaro Premium Lager.
FID Q (2)
Msanii wa bongo flava, Fid Q akizungumza na wakazi wa Mwanza wakati akitumbuiza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Bongo flava artiste Fid Q speaks to Mwanza residents during his performance at the Kili Music Tour concert held at Kirumba Stadium in Mwanza that attracted thousands of fans. The tour is sponsored by Kilimanjaro Premium Lager.
IZZO B
Msanii wa Bongo Flava Izzo Biznez akifanya vitu vyake wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Bongo flava artiste, Izzo Biznez perfoming during the Kili Music Tour concert held at Kirumba Stadium in Mwanza that attracted thousands of fans. The tour is sponsored by Kilimanjaro Premium Lager.
NYOMI (1) OMMY DIMPOZ (6)
Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz wakimakinika katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Vanessa Mdee and Ommy Dimpoz doing a collabo during the Kili Music Tour concert held at Kirumba Stadium in Mwanza that attracted thousands of fans. The tour is sponsored by Kilimanjaro Premium Lager.
RICH MAVOKO (8)
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rich Mavoko akipagawisha wakazi wa Mwanza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Renowned Bongo flava artiste, Rich Mavoko did not disappoint during the Kili Music Tour concert held at Kirumba Stadium in Mwanza that attracted thousands of fans. The tour is sponsored by Kilimanjaro Premium Lager.
VANNES MDEE (1)
Vanessa Mdee na Fid Q wakishirikiana kutoa burudani wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Vanessa Mdee and Fid Q making it happen during the Kili Music Tour concert held at Kirumba Stadium in Mwanza that attracted thousands of fans. The tour is sponsored by Kilimanjaro Premium Lager.
WEUSI (7) YOUNG KILLER (4)

Nyota Ndogo aelezea kwanini anahofia video yake ya ‘utupu’ inaweza kuvuja, na kilichomtokea hadi kurekodiwa akiwa mtupu.Soma kisa Kilivyokuwa

Muimbaji kutoka Mombasa, Kenya Nyota ndogo amejikuta katika hali ya wasiwasi baada ya kukutwa na mkasa wa karne hivi karibuni.
nyota
Nyota ameelezea kilichomkuta baada ya kuingia kwenye chumba cha hoteli ili abadili nguo, na kwa bahati mbaya alivua nguo zake mbele ya kioo cha chumba hicho bila kujua kioo hicho upande wa nje kinaonesha live bila chenga.
Kupitia akaunti yake ya Facebook Nyota Ndogo ameelezea kilichomsibu:
“yani nimekwenda show.nikapewa chumba chakubadili nguo.nimevua nguo zote najipaka mafuta pole pole kumbe najiangalia kwa kioo kumbe upande wapili naoneka kila kitu.yani nimekosa amani…aibu nilio iona mungu ndio anajua.sijui wamechukua video..haya ngoja tusubiri”.

nyota1

Hata hivyo Nyota amewapunguza wasiwasi mashabiki wake walio comment kumpa pole kwa kusema alibakiwa na nguo za ndani wakati hayo yanatokea.
“hapana nilibakisha cha ndani na nyonyo ilikua na nguo pia.kitu sielewi ni alienipeleka kubadili nguo ina maana hakujua nje naonekana?maana aliambia kioo hiki jiangalie mpaka miguu.”

nyota2

Tazama Picha Jinsi Diamond Platnum Alivyokutana na Meneja wa Trey Songz na Big Sean, Kevin Liles.Guess What?

Diamond Platnumz halali. Pamoja na mafanikio makubwa anayoendelea kuyapata, staa huyo anazidi kujitengeneza connection kali za kimataifa.
10296638_321755267974603_792512582_n
Picha ya juu: Diamond akiwa na Kevin Liles, meneja wa Trey Songz, Big Sean, Estelle na wasanii wengine

Katika kile kinachoonekana kuwa ni mazungumzo ya mwanzo wa safari ya kuelekea kuanza kufanya collabo na wasanii wa Marekani, Diamond amekutana na meneja wa Trey Songz, Big Sean na wasanii wengine wakubwa, Kevin Liles.
Mmoja wa watu waliopo kwenye timu ya Diamond, Salam wa SK Entertainment, ameshare picha nay a Diamond akiwa na Kevin Liles na kuandika: “Don’t Ask Me Whats Next…. Please 2 Days to go… VOTE FOR @diamondplatnumz for MTV MAMA Awards BEST COLLABORATION AND BEST MALE Kevin akiwa na Jay Z
Kevin Liles alikuwa rais wa Def Jam Recordings na makamu mkuu wa rais wa The Island Def Jam Music Group kuanzia mwaka 1999 hadi 2004.
kevin-liles-and-trey-songz1

Soma Kinachoendelea Juu ya Tuhuma ya Mume wa Flora Mbasha Kutoonekanan Mpaka Sasa

TAHADHARI! Wakati akiwa hajulikani alipo huku akishtakiwa kwa tuhuma ya ubakaji wa shemejiye, jeshi la polisi Bongo limemtaka mume wa mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha kujisalimisha mwenyewe.
TAHADHARI! Wakati akiwa hajulikani alipo huku akishtakiwa kwa tuhuma ya ubakaji wa shemejiye, jeshi la polisi Bongo limemtaka mume wa mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha kujisalimisha mwenyewe.

 
Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, akiwa na mume wake, Emmanuel Mbasha.
Habari za ndani zilieleza kuwa polisi wa Kituo cha Tabata-Shule, Dar ndiyo wamemtaka kujisalimisha baada ya binti anayedaiwa kubakwa kufungua jalada kituoni hapo lenye namba TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi namba TBT/IR/1865/2014 akidai kutendewa unyama huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili wiki mbili zilizopita).
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho ndani ya jeshi hilo, zoezi la kumsaka limeanza tangu Mei 19, mwaka huu aliposhitakiwa na shemejiye kituoni hapo lakini hadi gazeti hili linakwenda mitamboni Jumamosi jioni, jitihada zilikuwa hazijazaa matunda.

Tazama Picha za Red Carpet na Jinsi watu walivyotokelezea kwenye show ya Diamond Huko Houston Marekani








Moja Ya Picha Ilizo make Head Line Ni Hii ya Mh. Jakaya Mrisho Kikwete Kukutana Uso kwa Uso na Diamond Platnum Huko MANHATTAN, NEW YORK


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete masaa machache yaliyopita alipokutana na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz, Manhattan,

Tazama Picha Za Kuvutia Za Show Kubwa ya Diamond Platnum Ndani ya Jiji la New Jersey Marekeni

 All Star Club Elizabeth New Jersey Diamond akikamua licha ya show kuchelewa kuanza na wapenzi wa Diamond kushikwa na jazba wakitaka aendelee lakini ikashindika kutokana na muda wa kufunga club kufika.
 AJ nae akifanya yake baada ya kupewa nafasi ya ufunguzi katika show hiyo iliyofanyika New Jersey.
AJ Ubao na Dirty Hary wakishambulia jukwaa kwenye show ya kufubgua pazia iliyoanyika New Jersey na baadae Prezidaa wa Wasafi, Diamond Plutnumz kuwapagawisha mashabiki wake wa ukanda wa pwani ya mashariki.
Ni Rais wa Wasafi akishambulia jukwaa akiwa na madancer wake kwenye show ya kukata na shoka iliyofanyika New Jersey na kuvuta mashabiki kutoka kila kona ya pwani ya mashariki ambayo ni DC, PA, NJ, NY, CT, MA na kwingineko
Diamond mwanamuziki wa kizazi kipya anayekimbiza vibaya mno kwenye anga za Bongo Flava akipagawisha mashabiki wake New Jersey nchini Marekani.
Diamond na madancer wake wakijaribu kukata kiu ya mashabiki wake wa pwani ya mashariki.
 Wapenzi wa Diamond wakipagawa na show ya Diamond iliyofanyika All Star Club Elezabeth NJ.

May 24, 2014

Hebu Tazama Amazing Pichures za Pre-wedding dinner ya Kanye West na Kim Kardashian iliyofanyika jana Paris, ndoa kufungwa leo (May 24) Italy

Jana Ijumaa (May 23) Kanye West na Kim Kardashian waliianza ratiba yao kuelekea siku ya harusi ya mwaka inayosubiriwa kwa hamu kubwa kwa kufanya ‘pre-wedding dinner party’ huko Paris, Ufaransa huku ndoa yenyewe ikitarajiwa kufungwa leo.
kimye1
Maharusi wakiongea mbele ya wageni waalikwa

Jana mitaa ya Paris ilishuhudia pilikapilika za wageni na mapaparazi wakielekea eneo ilipofanyika sherehe ya chakula cha jioni kabla ya ndoa (pre-wedding dinner), iliyohudhuriwa na wageni wanaokadiriwa kufikia 100 wakiwemo dada zake Kim, Kourtney, Khloe, Kylie, Kendall na mama yake Kris Jenner na wageni wengine mbalimbali.
kimye3
Kim na ndugu zake

Usiku huo ulipambwa na burudani mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwimbaji aitwaye Lana Del Rey.
kimye2
Kwa mujibu wa ripoti, fataki zilitawala eneo la tukio, huku ikisemekana anga la eneo hilo siku ya jana lilikuwa ‘NO-FLY ZONE’, hakuna ndege yoyote iliyokatiza.
.
Chupa 1,000 za champagne ziliandaliwa kwaajili ya wageni waalikwa waliohudhuria.

Kwa mujibu wa Entertainment Tonight, maharusi watarajiwa Kimye waliwatangazia wageni waalikwa kuwa ndoa yao itafungwa siku inayofuata yaani leo Jumamosi (May 24) huko Italy.
kimye5
kimye6-kanye akilinda mali yake
Kanye akilinda mali yake

kimye7

May 23, 2014

Story Iliyomake Headline Tangu Asubuhi ni Hii ya Huyu Boss na Mmiliki wa Gest Mabibo Mwisho jijini Dar es Salaam, Amos Makelle kunaswa kitandani usiku wa manane na mfanyakazi wake aitwae Tina.

Amakweli dunia imekwisha! Watu wa Dar es Salaam wanasema uzee mwisho Chalinze, Dar es Salaam kila mtu baby, kauli hiyo ilitimia usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita baada ya mmiliki wa Gesti ya GLP ya Mabibo Mwisho jijini Dar es Salaam, Amos Makelle kunaswa kitandani usiku wa manane na mfanyakazi wake aitwae Tina.
Babu Amos Makelle baada ya kunaswa akiwa kitandani  na mfanyakazi wake aitwae Tina wakiwa tayari kuchepuka.
Bosi huyo na mfanyakazi wake walinaswa na mchumba wa Tina aitwae Salum Mbonde ambaye alipenyezewa umbeya huyo na mteja mmoja aliyekodi chumba kwenye gesti hiyo kwa ajili ya kufuatilia nyendo za wawili hao.
Baada ya mchumba wa Tina kupewa umbeya huo kuwa wawili hao walikuwa katika harakati za kuchepuka aliwawekea mtego na kuwashirikisha waandishi wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na askari wa doria.
BOSI ATOA SHINGO KUCHUNGULIA NOMA
OFM na mchumba wa Tina wakiwa wamelizingira eneo la gesti hiyo mishale ya Saa 8:17 usiku kukiwa kumetulia tuliii... mtonyaji aliyekodi chumba kwa ajili ya kazi maalum aliwatumia ujumbe mapaparazi wa OFM kuwa mzee Makelle aliyekuwa kwenye chumba chake alitoa shingo kama mara tatu na kuangalia kulia na kushoto kama kulikuwa na mtu aliyemuona.
Babu Amos Makelle bada ya kufumwa akiwa na mfanyakazi wake gesti.

Tazama Picha za Bibi Wa Miaka 65 Aliyekamatwa na Madawa ya Kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la sigara

 

 Huyu ni mzee, lakini tumeshangaa kuona bado ana nguvu za kutosha na tulishangaa baada ya kutoa kete 20 kwa mara moja katika awamu ya kwanza, jambo hili si rahisi kutokana na umri wake,”.

Bibi mmoja raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) amevunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA). Cole alikamatwa Jumatatu akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo. Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Alfred Nzowa zimesema pamoja na mbinu zake na kujiamini, mwanamke huyo alikamatwa kutokana na ushirikiano wa vitengo mbalimbali vya uwanja wa ndege. 
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani alisema mwanamke huyo alikamatwa Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia. 
Selemani alisema raia huyo aliwasili nchini Mei 15, mwaka huu na alikaa muda wote bila ya kuwa na shughuli yoyote, jambo ambalo lilitiliwa shaka na kumkamata. 


“Huyu mwanamke achana naye, akisimama mbele yako huwezi ukaamini kwa jinsi anavyojiamini. Alikuwa na mbinu mpya ya kufunga hizo kete. Kila moja ilifungwa kwa karatasi inayofanana na ganda la sigara,” alisema Selemani. 


Alisema mwanamke huyo alitumia mbinu hiyo ili asigundulike wakati akikaguliwa kwa mitambo maalumu inayogundua dawa za kulevya. 


Taarifa zaidi zinasema kuwa kutokana na mbinu yake ya ufungaji wa kete, mwanamke huyo alikuwa tayari amevuka hatua ya kwanza ya ukaguzi. 


Nzowa alisema baada ya kumhoji, mtuhumiwa huyo alidai kuwa aliingia nchini kwa ajili ya kutafuta soko la kuuza vipodozi na nguo. 


“Wakati tukiendelea kumhoji, Kikosi Kazi cha Kuthibiti Dawa za Kulevya kilibaini na kugundua kuwa alikuwa amemeza dawa za kulevya. 

May 22, 2014

Naomba Leo Niwasilishe Hii Taarifa Yenye Ukweli Kutoka kwa MamuAfrica Ni Jinsi Msanii Stara Thomas Akikiri ni Kweli Alikuwa Na Mahusisano na Marehemu Kambiana Wakati Marehemu Akiwa na Mke Wake ILA.....

 
Msanii Stara Thomas amefunguka kuhusiana na mahusino yake na aliyekuwa msanii wa bongo movie Adam Kuambiana aliyefariki wikiendi iliyopita na kuzikwa jana kwenye makaburi ya Kinondoni.
Stara amesema ni kweli aliwahi kuwa na mahusiano na Kuambiana lakini hata hivyo walitengena kutokana na kupishana baadhi ya tabia.

Anasema mahusiano yao yalianza walipokutana uwanja wa Taifa kwenye moja ya mechi iliyozikutanisha Bongo movie na Bongo flava na katika mahusinao yao hakuwahi kumwambia kama ana mke Zaidi ya kumwambia kuwa amewahi kuoa na ameachana na mke wake kwa talaka.

“Ni kweli nimewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Adam,uhusiano ambao ulifika mbali kiasi cha kutambuliwa nyumbani kwao kwa baadhi ya ndugu wakiwemo dada zake na hata babu yake mkubwa lakini hatukuweza kufikia kufunga ndoa kama tulivyokuwa tunafikiria,nakumbuka nilimuuliza kama ana mke akaniambia aliwahi kuoa na ameachana na mke wake”alisema Stara.


 

Amesema moja ya mambo makubwa ambayo walitofautiana ni pamoja na hasira kali kiasi cha kupelekea ugomvi mara kwa mara ,uvutaji wa sigara kupita kiasi wa Kuambiana ambaye hata alipokuwa akimueleza hakuwa akimuelewa,lakini pia kuna hitilafu ziliwahi kutokea kati yao walipokuwa safarini Zanzibar na Morogoro na mwisho akaona hawawezi kuishi kama mke na mume na kuamua kusitisha mahusiano.
 

“Unajua Adam alikuwa na kisukari sasa kwa kiasi kikubwa alikuwa anavuta sigara anapokuwa na stress zake na pia alikuwa mtu wa hasira sana,lakini kikubwa ni kutofautiana kwa baadhi ya tabia ambazo nikaona hatuwezi kuendelea na mahusiano yetu nikasitisha rasmi japo yeye mwenyewe aliomba kuwa atajirekebisha lakini ni vitu ambavyo vilikuwa vinajirudia nikaona hapana”Stara alisema.
Hata hivyo Stara amesema mbali ya kuwa na tofauti lakini Kuambiana hakuwa muhuni wa kubadili wanawake alikuwa ni mwenye kujiheshimu kwa kiasi kikubwa.