Hii Ni Interview aliyofanya na Sam Missago
Producer Castro [Castrol Ponella ] ametoka Jela miezi 5 iliyopita na leo
nilipata nafasi ya kuzungumza nae kuhusu muziki na maisha yake kwa
sasa. Ametoka 27 May 2013.
Ni producer aliyewahi kufanya kazi na rapper Queen Doren wa da Skendo, Mac 2 B, Fid q, Big Jahman, Spider na Akili The Brain.
Kwenye interview leo na sammisago.com Castro ameshukuru Wasanii na raia
wote waliomtembelea alivyo kuwa jela na kusema kuwa ulikuwa wakati mgumu
sana kwenye maisha yake na sasa yeye ni mtu tofauti.
Castro ameniambia wakati anakwenda jela palikuwa na studio tano tu Dar
es salaam, ameshanga sana kuona kila mtaa kuna studio na producers
wamekuwa wengi sana.
Alikuwa akisikiliza Bongo Fleva sana akiwa jela na alipenda sana
kusikiliza wimbo wa Darasa ft Winnie - Nishike Mkono Na ndio wimbo
uliompa faraja sana akiwa jela.
Castro amesema anataka sana kuendelea kutengeneza Hiphop
na msanii wa kwanza anataka kufanya nae Ni Darasa Na Fid q na ata taka
wafanye Collabo. Fahamu kuwa Darasa amefurahi sana kusikia hivyo na ombi
la Collabo na Fid q amelikubali sana na muda wowote yuko tayari
Kuhusu msanii anaye amini anafanya vizuri kwa sasa, Castro amesema
Anamkubali sana Diamond na ni kwa sababu Diamond anajituma sana ndio
maana anamafanikio.
Zembwela, Big Jahman, Fid Q, Snali, Baucha na Akili The Brain ndio walimtembelea sana Jela ndani ya hii miaka kumi iliyopita.
Castro ameniambia kuwa kilichobadilika sana kwenye bongo fleva ni show
nyingi zaidi,video za Bongo zimekuwa bora kwenye Production na muziki
mzuri unaofanywa na vijana wa Hiphop.
Castro amesema hajakata tamaa ya maisha na anampango wa kuanza kazi ya
muziki hivi karibuni na Jay Moe amempa Ushauri mzuri kuhusu maisha ya
muziki na game kwa ujumla.
Castro anapatika facebook kupitia Castrol Ponella.
From:Sammisago
No comments:
Post a Comment