Leo asubuhi (February 28) pande za Kinondoni Vijana Social Hall kulikua wasanii wa fani mbalimbali waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kuzindua kampeni ya kitaifa maalum kwa ajili ya kuishinikiza serikali kuwatambua wasanii kikatiba.
Licha
ya kuwa na shinikizo hilo lakini pia kutakuwa na maandamano ya amani
wanayotarajia kuyafanya ikiwa ni sambamba na kumpongeza Rais Jakaya
Kikwete kwa kumteua mmoja wao (hajafahamika bado) washiriki kuhudhuria
katika bunge la katiba.
tumepiga na nikki wa pili moja kati wasanii waliopo
mstari wa mbele kwenye movement hii
"Tumezindua
kampeni yetu ya kitaifa kushinikiza serikali itambue wasanii kama kundi
maalum kwenye jamii na kuingizwa kwa haki bunifu katika katiba hizo
ndio hoja zetu mbili tunazozipigia kelele" amesema Nikki wa Pili
lakini
pia ameendelea kusema "Tutafanya maandamano na kumfahamisha Raisi
Jakaya Kikwete kuwa sekta ya ubunifu inaingiza mapato kuliko sekta ya
Nishati na Madini ambayo inajadiliwa kila siku bungeni, lakini sekta ya
ubunifu imesahaulika"

No comments:
Post a Comment