NEW YORK,
Marekani
KUNDI la
muziki lilowahi kutamba hapo nyuma la Destiny's Child limetangaza kurejea upya
likiwa pamoja ambako wanatarajia kuachia albamu yao mpya itakayokwenda kwa jina
la ‘Nuclear’.
Kundi
hilo la muziki wa R&B lilitoa taarifa hiyo juzi baada ya kukaa kimya tangu
mwaka 2004 ambako ndipo walitoa albamu yao ya mwisho na kila mmoja kutawanyika
na kufanya kazi binafsi.
Albamu ya
‘Nuclear’ inatarajiwa kuwa na nyimbo 13 ambazo ziliwahi kutamba hapo nyuma kama
vile ‘Emotion’ na ‘Cater 2 U’ na baadhi ya kazi mpya ambazo zinatarajiwa kuwemo
ni pamoja na ‘Love Songs’ inayotarajiwa kutoka Januari 29.
Kazi hiyo
ya ‘Nuclear’ imetengenezwa chini ya utayarishaji wa Pharrell, akiwa
ameshirikiana na mwimbaji Michelle Williams.
Destiny's
Child, inaundwa na waimbaji kama vile Williams, Beyonce Knowles na Kelly Rowland
ambao walifanikiwa kutikisa ile mbaya katika anga za muziki na kuushtua
ulimwengu lakini baadaye kukaibuka malalamiko kutoka kwa weaimbaji wengine
wakilaumu kwamba nafasi kubwa anakuwa anapewa mwimbaji Beyonce kwa sababu
mkurugenzi wao alikuwa baba mzazi wa mwimbaji huyo.