Blogger Widgets

May 27, 2013

Endelea na Simulizi ya HATOOLEWA KAMWE sehemu ya Tatu Chini ya Utunzi wa ABDULMALIK SIRAJ,,,,,Ona Matokeo Yanafuata Baada ya Bi. Eliza kajifungua Mtoto wa Kike Ikiwa ni Muda Mrefu Kila Mimba Yake Inaharibika




SEHEMU YA TATU Mtunzi: ABDULMALIK SIRAJ
 Simulizi:NA HATOOLEWA KAMWE


****************
Ndipo nesi wazam akamtishia mzee kyashama kama iwapo hatoacha kupayuka kwa fujo atamtoa nje kwani alikua anawapigia kelele wagonjwa jambo ambalo lilimfanya mzee kiashama awe mpole atulie kama maji mtungin au ungezania ananyolewa kwajinsi alivyo nyea huku akikitazama kichanga chake...ndipo nesi alipo mgeukia mwanamke eliza na kumuuliza kisa ni nini!....eliza alisita kuongea akainua macho na kumuangalia mme wake machoni kwa muda mchache kisha akakigeukia kichanga chake na kuanza kukisemesha kama vile anamshtaki mume wake...''mwanangu hivi babaako ni wa kunikaripia na kunikaripia mbele za watu eti tu analazimisha uitwe KOKUSIIMA jina la mamaake mzaz kisa alimuahidi mtoto wa kwanza wa kike atakua mwajina wake...ss mwanangu uoni kama hayo majina ni yakizamani sana mimi nataka uitwe SUZANNA ..eti ndo kosa langu ilo mwanangu ndo niadhirike kias hiki kweli..''...maneno yale yalizua simanzi ndani ya moyo wa mzee kyashama akidi kunyong'onyea na kuinamisha kichwa chake kama mchicha ulonyauka kwa kupigwa na jua...ndipo nesi alipoingilia kati na kusema kuwa sio vibaya kwa mtoto kuwa na mjina mawili kwa ushaur tu jina la kwenye cheti chake cha kuzaliwa atumie SUZANNA... Kauli ile ya nes iliondoa ubishi na kulejesha fulaha kati ya wawili hao.....

****************

SUZANNA ni mtoto pekee wa mzee kyashama aloonyeshwa mapenzi ya dhati kutoka kwa wazazi wake walokua wakimtunza na kumlinda kama mboni ya jicho...jambo hilo lilimfanya suzi aish kwa furaha na kujivunia kuzaliwa ndani ndani ya nyumba ya mzee kyashama!..alipofikisha umri wa miaka tisa alianzishwa elimu ya msingi katika shule ya msingi TUMAINI..punde tu baada ya kuanza shule mschana suzi alikutana na kijana aitwae ERICK... Erick hakuwa mbali sana na alipokuwa akiishi suzi..erick alivutiwa sana na uzuri wa msichana suzi jambo lilimfanya ajiweke karibu sana na suzi,nakujikuta akiwa tayari kujitoa kwa namna yoyote ili mradi tu amfurahishe suzi..wawili hao walijikuta wakiwa karibu sana jambo liliwafanya hata wazazi kutoka pande zote mbili kufahamiana na kujenga urafiki pia...erick alimpenda sana suzi ila hakuwahi kumwambia..kwa upande wa suzi ilikuwa tofauti alimchukulia erick kama rafiki tu..suzi hakumpenda erick kutokana tofauti za kimuonekano,erick alikua anasura mbaya af alikuwa mweusi sana..wanafunzi wenzia walikua wakimtania kwa kumuita
MWILIMA maana yake GIZA..alikua anachukia sana akiitwa hivyo kama tunavyoekewa kwamba ukweli unauma...siku moja mwanamke eliza alikua amekaa kwenye kigoda huku akipembua mchele alipoinua macho kwa mbali aliona kundi la wanafunzi likiongozwa na erick wakiwa wamembeba mwanafunzi mwenzao ambae inaonesha kabisa kuwa aidha amepoteza faham au amefariki dunia...baada ya kuangalia kwa makin kwa mbali ndipo alipo gundua alobebwa ni mwanae suzi..ndipo alipoliachia ungo la mchele mpaka chini nakuanza kukimbia huku akizichanja mbuga kuelekea kwa mwanae suzi,....
KAMA UMEMISS SEHEMU YA KWANZA CLICK JUU KWENYE "SIMULIZI"

No comments:

Post a Comment