Katherine B. O'Connor akifanya dhihaka zake.
MWANAFUNZI mmoja wa kike wa Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon ameshitakiwa
Ijumaa kwa hali ya uvunjaji heshima na polisi wa kampasi baada ya Askofu
Katoliki kulalamika kuhusu kutembea kwake hadharani akiwa uchi kuanzia
kiunoni kwenda chini huku kavalia kama Papa.
Mwanafunzi mmoja wa kiume ambaye alikuwa uchi pia ameshitakiwa, lakini
haikufahamika mara moja alichokuwa akifanya wakati wa gwaride la sanaa
ya uch
oraji la majira ya bamvua ya Shule ya Pittsburgh mwezi uliopita.
Rais wa Chuo hicho, Jared Cohon alisema Ijumaa iliyopita kwamba
mashitaka hayo madogo yalikuwa yamefunguliwa huko Allegheny County dhidi
ya wanafunzi hao wawili na kwamba shule hiyo haitachukua hatua zozote
zaidi za kinidhamu.
Alisema shule hiyo imebariki kujieleza kisanii lakini kujianika uchi hadharani ni kinyume cha sheria.
"Kuna ushindani wa thamani katika suala hapa: Carnegie Mellon inakusudia
kuwa sehemu ambako mawazo yanaweza kuwasilishwa na kujadiliwa kwa
uwazi, lakini pia ambapo watu wa historia zote, dini, na imani kujisikia
wanakaribishwa na kupewa msaada," alisema Cohon.
Askofu David Zubik wa Dayosisi Katoliki ya Pittsburgh alilalamika baada
ya gwaride hilo Aprili 18, ambapo mwanafunzi huyo wa kike - huku nywele
zake za sehemu za siri zikiwa zimenyolewa kwa alama ya msalaba -
alirusha kondomu kwa watazamaji. Cohon aliomba radhi wiki iliyopita kwa
onesho hilo.
Chuo hicho hakikuwataja wanafunzi hao wawili. Rekodi za mahakama
zinaonesha wanafunzi hao Katherine B. O'Connor, miaka 19, kutoka
Pittsburgh, na Robb S. Godshaw, miaka 22, kutoka Wilmette, Illinois,
walishitakiwa na polisi wa kampasi kwa tukio la uvunjaji heshima.
Hakuna mwanasheria aliyekuwa amejitokeza kumtetea yeyote.
Si O'Connor wala Godshaw aliyejibu ombi la kutoa maoni yoyote kuhusiana
na suala hilo, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa kwa mara ya kwanza Juni
10, mwaka huu.
Zubik alisema katika taarifa Ijumaa kwamba Chuo Kikuu hicho kinalichukulia 'tukio hili lisilotarajiwa' kwa uzito wa kipekee.

No comments:
Post a Comment