Blogger Widgets

January 26, 2013

Jini Kabula atoa Maelezo ya yeye kuwa anaonekana Hotelini akiwa na Mpenzi wake wa Zamani Mr. Chuzi

LICHA ya kumwagana, mwigizaji mwenye mbwembwe nyingi kila kukicha ambaye ni mwajiriwa wa Kampuni Tuesday Enternment, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, amefunguka kuwa akitaka kujadili mambo ya mtoto aliyezaa na Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ huwa wanakwenda hotelini.  
Akizungumza na Weekely Star Exclusive, Jini Kabula alisema kuwa pamoja na kwamba mapenzi yao yalikwisha zamani, bado wanapata muda mrefu wa kujadili kuhusu mtoto wao wakiwa wamejifungia kwenye cha hoteli yenye utulivu.

“Linapokuja suala la mtoto, huwa tunatafuta sehemu ambayo ni tulivu ili kujadili  mambo ya mtoto. Tunakaa na kuongea mambo mbalimbali kwa ajili ya mtoto wetu, Salma,” alifunguka Kabula.
 Alipoulizwa kama wanapokutana huwa wanavunja amri ya sita, Kabula aliruka futi mia moja na kusema kwamba mapenzi yalishakwisha na kinachowaungnisha kwa sasa ni suala la mtoto tu.
“Tukiwa hotelini na Chuz ni kwa ajili ya mtoto wetu maana sisi tukisikilizana, mtoto wetu atakuwa kwenye mazingira bora,” alisema Kabula kwa kujiamini.
Alipotafutwa Chuz ili kuthibitisha habari hizo, kilongalonga chake cha kiganjani kiliita bila kupokelewa.