Baada ya taarifa za uhakika kutoka kuhusu kifo cha Rais wa Venezuela Hugo Chavez amefariki dunia, kupitia taarifa ambayo imetolewa na kituo cha Al Jazeera Rais Barack Obama wa Marekani amesema nchi yake imehamasika kuanza mazungumzo ya uhusiano mpya wa nchi hizo mbili.
Rais Hugo Chavez amefariki akiwa
na umri wa miaka 58 akisumbuliwa na kansa na taarifa yake kutangazwa
usiku wa kuamkia march 6 2013 ambapo kifo chake kilitangazwa na makamu
wa Rais Nicolas Maduro ambae sekunde 40 baada ya kuanza kutangaza kifo
hicho alishindwa kuzuia hisia zake na kulazimika kusimama kuongea kwa
muda kutokana na machungu.
