Wakati ile Event kubwa ambayo imewakutanisha wale mastar ambao
wametoklezea katika orodha ya Time ya wati 100 wenye influence zaidi
duniani ikiwa imefanyika huko New York Marekani na Rapa Jay Z akiwa ni
moja kati ya watu wakubwa waliomiss tukio hili, Tayari imeshafahamika ni
kwasababu gani mkali huyu hakuwawepo katika tukio hili kubwa.
Jay Z pamoja na Beyonce na mtoto wao Blue Ivy, kwa mara nyingine kati
ya zile chache sana ambazo zimewahi kutokea, wameonekana waziwazi huko
Paris Ufaransa wakiwa wanapata msosi wa mchana katika mgahawa mmoja
maafuru, ikiwa ni Tym ya pamoja ya familia mbali na majukumu mbalimbali
ambayo mara nyingi huwa yanawaweka mastar hawa mbali mbali.





