Blogger Widgets

April 1, 2013

Judith Wambura aendelea Kudili na Radio Ya watu anaowaita Ni Wanafiki

.


Redio hii ni wanafiki
>> Autaja wimbo wa Joto Hasira akiwa na Prof Jay
>> Asema litakalokuwa na liwe na hatarudi nyuma
 Siku chache baada ya kutoa wimbo mpya wa Joto Hasira, staa wa muziki, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ameonyesha kuwa na hasira za ukweli baada ya kushutumu kituo cha redio kuwa kinatoa upendeleo kwa baadi ya wasanii na ‘kuwabania, wengine.

Kupitia ukurasa wake katika mtandao wa Twitter wa twitter.com/JideJaydee, msanii huyo hajataja jina la kituo hicho lakini inavyoonekana hatua hiyo imefikiwa baada ya wadau hao ‘kuupotezea wimbo wake huo mpya aliomshirikisha Joseph Haule ‘Prifesa Jay’

Jaydee ameonekana kuwa na hasira na kuandika baadhi ya maneno kama ifuatavyo:-

·         Redio ya watu isipopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhulu Nakunywa maziwa daily, I will survive. 

·         Kili me if u can, am on Fire, siogopi Ng’ooooo Jipangeni. 

·         2013 no more bullshits, we fight mpk jasho la mwisho. 

·         Mmetiwa petrol inanuka mioyo imeshawawaka kabla ya kutiwa kibiriti. Maamuzi magumu yalishafanywa na wenye roho za kutu fanyeni ku top up.

·         Tuki stuck ndo mwisho wetu na adui anashangilia, ni kupambana tu mpk mwisho radio ziko nyingi mbona. 

·         @Profesa_Jay Iwe Joto au Baridi lazima kushinda mbwai, mbwai tu. Hakuna kuremba. 

·         Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava Sasa hata wasioijua Hip-hop nao wana beef na Bongo flava! Damn!! 

·         My name is Judith Wambura Habash!! Hio imeandikwa kwenye passport. Gmorning. 

·         Vinyoka nyamazeni acheni Anaconda aongee. 

·         Hee! Kuna wajinga wanadhani nili tweet nikwa nimelewa, nilimaanisha na msimamo ni huo. Stasema ooh kuna mtu ka hack ac yangu nooo it’s   me. 

·         Kuna DJ flani alikuwa akipiga nyimbo nilizoshirikishwa akifika sehemu nilioimba mimi anakata verse yangu nimtaje??