MREMBO Sikujua Hassan, mwenye ujauzito unaokadiriwa kuwa na umri wa miezi sita, alinaswa akifanya ukahaba, Buguruni, Dar es Salaam.
Sikujua, alinaswa na polisi kisha kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Sokoine Drive, Dar es Salaam ambapo alikiri kosa la kujihusisha na ukahaba.
Baada ya kukiri kosa, Hakimu Mkazi, William Mutaki, alimhukumu kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya shilingi 20,000.
Hata hivyo, Sikujua hakuweza kulipa faini, kwa hiyo aliamriwa kwenda gerezani pamoja na ujauzito wake.
Sikujua amepangiwa kutumikia adhabu hiyo kwenye Gereza la Segerea, Dar.
Watu mbalimbali waliokuwepo mahakamani hapo, walimsikitikia Sikujua kutokana na hali yake.