SONG:
MUZIKI GANI
ARTIST:
NEY WAMITEGO FEAT DIAMOND
PRODUCER:
MR TOUCH
CHORUS
Hivi nyi ma mc mnachoimba kitu gani,
mara bangi mara matusi sa ndo muziki gani (diamond).
Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney) X2
Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney) X2
DIAMOND
Hata bibi yangu mi aliniambia ,
mwanamke anahitaji kubembelezwa
Kupetipeti matunzo pia, ukienda rafu
utampoteza,
Muziki ni mfano wa binti muzuri,
Na ndio maana namtunza kwa vazi na uturi
NEY
WA MITEG
Aaah piga kimya, we ndo haufai
kabisa hauna maana
Wabana pua kila siku mnarogana, bibi
yako alikuambia muziki ni kama binti
Mbona unawachezea unawatema kama big
g
Mara wema, mara Jo keti, mara Naj,
mara Penny, je mnafanya mziki mpate mabinti
DIAMOND
Uuuhhuuuu, hata wazee wazamani, walishasemaga
kazi na dawa
Chamuhimu jukwaani, ni kuhakikisha
wanapagawa,
Kwa michezo ya kuringa ringa ndo huwa wanadata
Badilika usiwe mjinga, utawakamata
CHORUS
Hivi nyi ma mc mnachoimba kitu gani,
mara bangi mara matusi sa ndo muziki gani (diamond).
Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney) X2
Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney) X2
NEY
WA MITEGO
Muziki wenu ushirikina ndio
umetawala, q chilla analalama anasema umemroga
Mganga wako aliekutoa umemkimbia
hujalipa, bila skendo za magazeti basi
huskiki
DIAMOND
Mi ni mti wenye matunda, milele
siogopi kupigwa mawe
Ubaya wenu wengi kayumba, elimu
mliitupa sandakalawe
NEY
WA MITEGO
Bado hujanishawishi, bongo fleva
inanipa kichefu chefu
Kwanza nyie malimbukeni wa umaarufu
Mnalenta maringo mpaka kwa mashabiki
, Wabana pua nyie watoto sio riziki,
Mnavaa nguo za dada zenu, zinawabana
mapaja nyie makaka duu
Nimewanyamazisha, brazameni
vipi we bado unabisha
DIAMOND
Mi nnamengi nnayajua, ila we ni
mtemi utaanzisha utata
Michezo yenu kutoboa pua, bora
ninyamaze usinipige mbata