Blogger Widgets

May 13, 2013

Linex AMliza Mama Yake Tena Mbele ya Umati


Msanii Linex ambae amejizolea mashabiki kibao kutokana na umahiri wake katika kutumia sauti yake, jana amemliza mama yake mzazai pale alipokuwa akifanya show yake ya bure mkoani alipozaliwa, Kasulu, Kigoma.
Tangu Linex alipoanza safari yake ya muziki takribani miaka 3, mama yake mzazi hajawahi kumuona na kumshuhudia mtoto wake live akifanya show.Ni katika uwanja wa ambapo mama alimshudia mtoto wake akiwa amejaza umati wa watu kuja kumshuhudia akifanya show, ndipo alipokutana na umati huo na jinsi kila mmoja alivyokua akimshangilia na kujikuta akimwaga machozi na kumsababisha Linex kuangua kilio pia akiwa mbele za mashabiki wake.
Linex aliamua kufanya show hiyo bure mjini kwao kwa ajili ya kutoa sapotio kwa wanao msapoti..

"yaani nimeshangaa sana kukuta umati wa watu uwanjani, unajua Kasulu ni mji mdogo sana so kukuta watu wote wale sijui hata wametoka wapi, ki ukweli mama yangu hajawahi kuniona nikifanya show, jana ndio ilikua mara yake ya kwanza, na alishangaa sana kuona watu ni wengi na wanashow love ya hatari..wakati mi naimba pale, nilimuona mama yangu na furaha mpaka anatoka machozi, ki ukweli nilijikuta na mimi naangua kilio tu, ila ilikua nzuri sana na watu wamefurahi sana" amesema Linex



No comments:

Post a Comment